KIKOTI EDUCATION CENTRE

KIKOTI EDUCATION CENTRE

Alhamisi, 27 Oktoba 2016

Uongozi wa Kikoti Education Centre wapongezwa

picha: wanafunzi wa kikoti education centre wakiwa shule ya sekondary mazombe 
pongezi hizo zilizotolewa pale wanafunzi kutoka kikoti education centre walipotembelea shule ya sekondary mazombe katika ziara ya kimasomo iliyohusisha mashindano ya debate(mdahalo wa lugha ya kiingereza uliokuwa unaohoji je elimu na pesa kipi bora (is education batter than money)?
awali kabla ya kuanza mashindano hayo mkuu wa shule hiyo alianza kwa kuwakaribisha wageni wake kwenye ofisi yake kwaajili ya kusaini kitabu cha wageni na baada ya hapo akawakabidhi wageni hao kwa mwalimu wa taaluma kwaajili ya kuwaonesha mazingira ya shule na namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika shuleni hapo.


Baada ya mwalimu wa taaluma kuambatana na head boy(kaka mkuu) na head girl(dada mkuu) mashindano yalianza kwa mwenyekiti wa mdahalo huo kukaribisha motion mover(yaani mfafanuzi wa debate) kwaajili ya kuelezea debate. baada ya hapo mwenyekiti wa mdahalo aliruhusu debate kuanza kwa kuelezea kwamba kikoti education centre watakuwa proposer side na mazombe secondary watakuwa opposer side
 wazungumzaji wote walionekana wakijiamini kwa kuongea point zenye mantiki na zilizovuta hisia kubwa kwa watazamaji na wasikilizaji wa debate hiyo na wenyekiti alifanikiwa kumaliza debate mnamo saa nane na nusu jioni

Baada ya saa nane mwnyekiti alimkaribisha jaji wa debate hiyo kwaajili ya kutoa kasoro na kutaja mshindi wa debate hiyo ndipo jaji akathibitisha kwamba kikoti education centre wakatajwa kuwa washindi wa debate hiyo kwa point kumi na tatu dhidi ya mazombe waliopata point tisa
 baada ya hapo walimu walikalibishwa kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ndipo kwa niaba ya kituo mwalim edgar msamba aliweza kuwazungumza na wanafunzi hao ambapo alisisitiza wanafunzi wa shule zote mbili kuwa makini sana na masomo nakuongeza jitihada zao katika masomo yao.
pia aliwataarifu rasmi wanafunzi hao kwamba kituo kitaendelea kutoa huduma wa tuition na kuwakaribisha wanafunzi hao kwenda kusoma kituo bora chenye walimu bora na wenye uwezo stahiki na kumalizia kwa kusema kuna watu watakuja kuwarubuni hapa msidanganyike na maneno yao maana hata wenzenu pre form one mnaowaona leo walidanganyika na kwenda kwa bwana mmoja lakini saa wanasumbuka kuja kulipa ada kwetu mara mbili kutokana na elimu wanayoipata waliko
 ndipo kwa heshima na taadhima mwl kikoti akasimama na kwenda kumkabidhi zawadi mwanafunzi mmoja wa mazombe secondary school aliyeonesha uwezo mkubwa katika kuzungumza zawadi hiyo ilikua ni kitabu halisi kutoka kikoti education centre
 picha: Baadhi ya wanafunzi kutoka kikoti education centre wakifuatilia mdahalo huo
 Picha: ni baadhi ya wanafunzi wa mazombe sekondari wakiendele kusikiliza mdahalo
 Picha : ni baadhi ya viongozi wa debate wakiendelea kutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha taratibu na sheria za debate zinazingatiwa

Maoni 1 :